MAJALIWA AWAAGIZA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI KUFUFUA MADARASA YA MEMKWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanafufua madarasa kwa ajili ya Mpango wa Elimu ya Msingi kwa walioikosa (MEMKWA) ili kusaidia kupunguza ongezeko la watu wazima wasiojua kusoma na kuandika. Ametoa agizo hilo leo (Jumatano Juni 9, 2021) wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Kuadhimisha Miaka 50 ya